KESHA LA ASUBUHI JULAI 18/07/2025 Tu Wachungaji Wasaidizi
Tu Wachungaji Wasaidizi Julai 18 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.” — Mathayo 7:15 Kadiri unavyomtazama Yesu na upendo Wake usio na kifani kwa juujuu, ndivyo unavyoshindwa kubadilishwa ili kufanana Naye. Utajiona bora machoni pako mwenyewe, na hivyo kuwa na kujiamini na kuridhika na jinsi ulivyo. Ufahamu sahihi wa Yesu, kumtazama daima kama Mwanzilishi na Mkamilishaji wa imani yetu, hutupatia mtazamo wa kweli wa tabia ya Mkristo kiasi kwamba huwezi kushindwa kufanya makadirio sahihi ya maisha na tabia yako tofauti na zile za Mfano wetu mkuu. Kukamilishwa kwa ajili ya kazi yako ni shughuli ya maisha ya kila siku — kazi ngumu, mapambano ya karibu na mazoea ya kibinadamu, mielekeo ya kurithi. Inahitaji juhudi ya mara kwa mara, ya dhati na ya uangalifu ili kuitazama na kuidhibiti nafsi, kumweka Yesu kuwa mashuhuri na ubinafsi kutoonekana. Ni muhimu kuchunguza eneo dhaifu katika tabia yako, ku...