_KESHA LA ASUBUHI *JUMATATU, JULAI 14 2025*
KONDOO WALIOPOTEA NI MZIGO WA PEKEE
*Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone*?
_Luka 15:4_
▶️ *Ni kazi muhimu sana kushughulika na akili za wanadamu. Mwanadamu ni mali ya Mungu, na malaika wanaangalia kwa shauku kubwa ili kuona namna ambavyo mwanadamu atashughulika na wanadamu wenzake.*
▶️ Viumbe wa mbinguni wanapoona wale ambao wanadai kuwa wana na binti za Mungu wakifanya jitihada kama za Kristo ili kusaidia wakosaji, wakiwaonesha roho ya upole na huruma waliotubu na walioanguka, malaika wanawakaribia, na kuwakumbusha maneno yale ambayo yatatuliza na kuinua nafsi. Malaika watakatifu wanatufuatilia kila mmoja wetu. Hatupaswi kuwadharau watu wa Mungu walio wadogo zaidi, tusitafute heshima kwa yeyote kwa ajili yetu. Malaika ni roho zihudumuzo zilizotumwa kuwahudumia wale ambao watakuwa warithi wa wokovu. Je! tutapata fadhila ya kushirikiana na wenye hekima wa mbinguni? Je! Mungu atatukubali kuwa wabeba nuru kwa ulimwengu?
▶️ *Yesu Kristo amechukua nafasi ya yule aliyekuja kutafuta na kuokoa kile kilichokuwa kimepotea, na ameuinua ulimwengu kiasi kwamba alikufa ili kuuokoa, ili kumrudisha kondoo mmoja aliyepotea zizini.* Yesu ametoa uhai wake wa thamani, uangalizi wake binafsi, kwa watoto wa Mungu walio wadogo zaidi; na malaika walio hodari hufanya kituo wakiwazungukia wote wamchao Mungu. Kwa hiyo tuwe waangalifu, na kamwe tusiruhusu wazo moja hafifu kushughulisha akili kuhusu mmoja wa watoto wa Mungu walio wadogo. Tunapaswa kuwaangalia waliokosea kwa kutaka kuwasaidia, na kusema maneno yenye kuwatia moyo walioanguka, na kuogopa isije ikawa kwa matendo yasiyo na busara tukawaondolea mbali na Mwokozi mwenye huruma.
▶️ *Wale wanaompenda Yesu watawapenda wale ambao Yesu aliwafia. Ikiwa wengi wa wenye dhambi walio karibu nasi wangepokea nuru ambayo imetubariki sisi, wangefurahia ukweli, na kuwa mbele ya wengi ambao wamekuwa na uzoefu wa muda mrefu na faida kubwa. Wachukueni kondoo hawa waliopotea kuwa mzigo wenu maalum, na mzitunze roho kama wale ambao wanalazimika kutoa hesabu. Usijimakinikie mwenyewe, bali upaze sauti kwa shauku kuu na ya dhati, "Tazama Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu." Huu ni ujumbe wa Mkristo kwa ulimwengu. Hii ndiyo hoja yenye nguvu. Uhimize moyo wako kuweka juhudi za dhati ili kuzishawishi roho zinazoangamia kukaza macho yao kwake Yeye aliyeinuliwa juu ya msalaba; na ukumbuke kwamba unapofanya hivi, malaika wasioonekana wanaweka ushawishi moyoni, na kuiongoza nafsi kumwamini Yesu. Mwenye dhambi anawezeshwa kumwona Yesu kama alivyo - ni mwingi wa upole, huruma na upendo na anasema, "Na unyenyekevu wako umenikuza*" _(Zaburi 18:35) (The Review and Herald, Juni 30, 1896)_.
*MWENYEZI MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*
Comments
Post a Comment