KESHA LA ASUBUHI JULAI 12 2025 " THAMANI YA KONDOO ALIYEPOTEA"

Thamani ya Kondoo Aliyepotea

"Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba Yeye alitupenda sisi." — 1 Yohana 4:10

Mafarisayo walidai kwamba kama Yesu angekuwa nabii wa kweli, angepatana nao, akatangaza amri na kanuni zao, na kuwatendea watoza ushuru na wenye dhambi kama wao walivyowatendea. Lakini katika kumtoa Mwanawe kufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, Mungu alionesha thamani aliyoweka juu ya mwanadamu. Kwa kumtoa Yesu kwa ulimwengu, alitoa zawadi bora kabisa ya mbinguni.
Kwa sababu ya dhabihu hii ya gharama kubwa, shukrani kubwa zaidi inadaiwa kutoka kwa kila nafsi.

Bila kujali taifa, kabila, au lugha—iwe mweupe au mweusi—mwanadamu ameumbwa kwa sura ya Mungu. Na somo sahihi la mwanadamu kujifunza ni mwanadamu mwenyewe, kwa sababu amenunuliwa kwa damu ya Yesu. Kudharau au kuchukia taifa fulani ni kudhihirisha tabia ya Shetani.

Mungu ameweka thamani ya kipekee juu ya mwanadamu kwa kumtoa Yesu kupitia maisha ya fedheha, umaskini, mateso, na kifo—ili kondoo Wake aliyepotea aweze kuokolewa. Je, ni ajabu kwamba mbingu zote zinavutiwa na fidia ya mwanadamu?
Elfu kumi mara elfu kumi, na maelfu ya maelfu ya malaika wamepewa kazi ya kupanda na kushuka kwenye ngazi ya ajabu ili kuwahudumia wale watakaokuwa warithi wa wokovu.

Malaika hawaji duniani kushutumu, kuharibu, kutawala au kutafuta heshima. Wao ni wajumbe wa rehema, wakishirikiana na Kapteni wa jeshi la Bwana pamoja na mawakala wa kibinadamu wanaojitolea kutafuta na kuokoa kondoo waliopotea. Wanaagizwa kupiga kambi kuwazunguka wale wanaomcha na kumpenda Mungu.

Huruma yote ya mbingu imetolewa kwa ajili ya kondoo waliotangatanga mbali na zizi. Kama Mafarisayo wangefanya kazi kwa kupatana na Mungu badala ya kushirikiana na adui wa Mungu na mwanadamu, wasingewadharau wale walionunuliwa kwa damu ya Yesu.
Giza la udanganyifu linapovunjwa kutoka kwa akili ya mwanadamu, mwenye dhambi anapotazama Kalvari na kuona dhabihu ya ajabu iliyotolewa ili kuokoa jamii iliyoasi na kuharibiwa, huguswa na upendo wa Mungu—na anatubu.

"Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba Yeye alitupenda sisi."

Hebu tujitahidi kuelewa upendo huu—japokuwa kwa sehemu tu—ili tuanze kuelewa huruma iliyodhihirishwa kwa mwanadamu aliyeanguka. Tunawezaje kutazama msalaba na kuendelea kuishi kimoyomoyo?
Kwa kumtazama Kristo, mwanadamu hubadilishwa na kufanywa upya katika tabia, toka utukufu hata utukufu. Anaingia katika pambano la nuru dhidi ya giza.

Mtazame maskini mwenye dhambi aliyechakazwa na maisha—yeye ndiye kondoo aliyepotea ambaye mchungaji anamtafuta.
Mtazame msalabani… yule kipofu aliyerudishiwa kuona kwa huruma ya Mchungaji wa kweli ndiye yule aliyedharauliwa na Mafarisayo waliojikinai. Walimwona kama mtu asiyestahili chochote… bali chuki.

(The Signs of the Times, Novemba 20, 1893)


MUNGU AKUBARIKI🕊️

Comments

Popular posts from this blog

KESHA LA ASUBUHI JULAI 16/017/2025

KESHA LA ASUBUHI 15/07/2025 Kumpata Kondoo Aliyepotea

KESHA LA ASUBUHI JULAI 18/07/2025 Tu Wachungaji Wasaidizi