✨ Karibu katika blogu ya Kweli za Thamani



KARIBU"


Hii ni  Blogu ya Maisha, Imani, na Kusudi la Umilele

Karibu sana kwenye  "Kweli za Thamani", blogu iliyoanzishwa kutoka moyoni kwa makusudi ya kutafakari, kujifunza, na kushirikiana kweli za neno la MUNGU zinazotupatia uzima wa milele. Jina lenyewe linabeba kusudi kuu la kuhifadhi na kusambaza hazina ya kiroho ambayo hu n'gaa ukiangaza maisha ya kila siku kwa mwanga wa Neno la Mungu.

Mimi ni Hebroni ,  Ni  Mume, baba, Mchungaji, na mwanajamii mwenye kiu ya maarifa na huduma. Katika safari yangu ya imani imenifunza kuwa hakuna msingi imara unaozidi Neno la Mungu, na hakuna urithi bora kwa familia zetu kuliko kweli zinazoishi.


Katika blogu hii tutakuwa na mambo yafuatayo:

Makala mbalibali ya kiroho yanayoendana na wakati huu wa mwisho wa historia ya dunia.

Tutajifunza pomoja mafundisho ya Biblia kwa ajili ya familia, safari ya kiroho katika imani, na mtindo na chaguzi za maisha ya kila siku.

tutashiriki kwa pamoja nyenzo za kujijenga, kutafakari, na kutuinua katika viwango vya juu vya maisha ya kiroho, kijamii, kimwili na kiakili


Sauti ya Mungu bado inaita. Na Kweli za Thamani ni jukwaa dogo lakini lenye uthubutu wa kuisikiliza, kuihifadhi, na kuishiriki kwa upendo na uaminifu kweli hizi za thamani kutoka kwa Mungu.


Karibu katika safari hii ya nuru. Tafakari, shiriki, na tembea nami kwenye njia ya kweli isiyochakaa.

Comments

Popular posts from this blog

KESHA LA ASUBUHI JULAI 16/017/2025

KESHA LA ASUBUHI 15/07/2025 Kumpata Kondoo Aliyepotea

KESHA LA ASUBUHI JULAI 18/07/2025 Tu Wachungaji Wasaidizi