Hatari Ya Wengi Wetu Leo Kupuuzia Sauti Ya Mungu Inayozungumza Nai Kila Uchao
Sehemu ya Kwanza
Mungu Anazungumza Kupitia Neno Lake
๐ “Yeye anayenikataa Mimi, asiyeyakubali maneno Yangu, anaye wa kumhukumu—Neno lile nililosema ndilo litamhukumu siku ya mwisho.”.” — Yohana 12:48
๐น Neno la Mungu — Sauti halisi ya MUNGU Inayozungumza
Yesu mwenyewe anatoa angalizo la hukumu kwa wale watakaomkataa yeye, na mhukumu aneyetajwaa hapa ni neno. kwa nini neno ndilo lihukumulo? tunaporejea (Yohana 1:1-4, 14) Kama Neno la Mungu (Logos): Yesu ndiye ufunuo wa asili wa Mungu kwa wanadamu — si tu msemaji wa Mungu, bali Neno lenyewe. Kwa Kigiriki, "Logos" lina maana ya hekima, mantiki, na ufunuo. kama yesu ni neno pale tunapolipuuzia neno la Mungu ni dhahiri kuwa tunampuuzia Yesu mwenyewe. na somo hili litajenga msingi wa kulitambua na kuliheshimu na kufanya neno la Mungu liwe sehemu katika maisha yetu yenye tija kwa ajili ya kutuandaa na umilele.
Kila siku sauti ya aliyeumba mbingu na nchi (Mungu mwenyewe) Inazungumza. Sauti yake haitoki kwa mshindo usiosikia; inatoka kwenye Neno lake, lilioandikwa kwa upendo, maarifa, na maonyo ya uzima. Lakini leo, sauti hiyo inapuuziwa kwa ujasiri usio na hekima.
Watu wengi wanatafuta mafundisho kutoka kwa wanadamu viongozi, mila, mapokeo ya kidini yasiyo na msingi wa neno la Mungu na huzidi kupuuza maneno ya Biblia. Neno ambalo lilipaswa kuwa dira, limewekwa pembeni na watu leo hii hufuata dira za wanadamu na ushawishi wa mvuto wa kiulimwengu. Kwa sababu hiyo, maarifa yanayookoa maisha yanapotea, kwa kutojua wengi hata wanaodai kumfahamu Mungu wapo katika giza na roho za wengi zinaangamia kwa kunaswa na mtego wa mwovu ibilisi, kama matokeo ya kutotaka kusikia sauti yaa Mungu.
Biblia (neno la Mungu) haipo ili isomwe kama gazeti au historia ya dini; ni barua ya Mungu kwa wanadamu. Kila mstari ni sauti ya Mungu ikisema: “Njoo.” Lakini wengi wanasikia — hawatii. Wanaelewa — hawafuati. Hii si tu kupuuza maandishi, ni kumpuuza Mnenaji mwenyewe ambaye ni MUNGU.
๐น Maarifa Ya Biblia Si Chaguo — Ni Uhai
Biblia neno la Mungu lipo na Mungu hutoa fursa ya Kuchagua. (Kumbukumbu la Torati 30:19)Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako
Hebu tafakari hili: Watu wanaangamia si kwa sababu ya upumbavu, bali kwa kukosa maarifa ya kweli, Nenp la Mungu/Sauti Ya Mungu mwenyewe, na hufanya mara nyingi kwa makusudi. wengi wetu leo wanaamua kusikiliza wanadamu na mapokeo kuliko Mungu. Hii ni hatari kubwa, kwa maana maandiko yanasema wazi: kudharau sauti ya Mungu, matokeo yake ni Kuangamia
“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.” — Hosea 4:6
Je, ni kweli kwamba tunajua Biblia lakini hatuishi kwa Neno lake? Je, tunahudhuria ibada lakini hatujui sauti ya Mchungaji Mkuu?
๐น Neno Liko Tayari kila wakati — Lakini Tunalisikia Kwa mazoea tunapokwenda kanisani
Watu wengi wanasikiliza sauti za walimu, mahubiri ya kuvutia, makundi ya kidini — lakini hawachunguzi kila neno kutoka kwa kinywa cha Mungu. mara nyingi tunafanya ibada bila uhusiano, tunaishi kwa mazoea bila mabadiliko, tunadai kuwa tuna imani bila maarifa. Huu ni mtindo mfu kwa mkristo — usiosalimisha moyo kwa sauti ya Mungu.
๐น Mwito wa Siku ya Leo: Bwana anatuhitaji ttafute kila siku kila wakati fursa ya kuzungumza naye. na tuafoyaangalia maisha yetu:-
Je, kweli tunasikiliza sauti ya Mungu au tunafuata urithi wa wanadamu?
Je, Biblia ni mwongozo wa maisha au ni mapambo ya ibada?
Je, tumenyenyekea chini ya Neno au tunachagua yale yanayotuonea huruma na yale tunayoyapenda?
Sauti ya Mungu iko wazi — iko kwenye Biblia. Na ukiikataa leo, maandiko yanasema “unae wa kukuhukumu.”
Kesho, tutachapisha Sehemu ya Pili: Wengi Wanasikiliza Sauti za Watu, Siyo za Mungu, tutaichunguza kwa kina jinsi mapokeo na maoni ya wanadamu yanavyozuia uzima wa milele.
Fuatana nasiTuendelee kujenga ufahamu juu Maandiko neno la MUNGU. ๐๐️
Comments
Post a Comment