Posts

KESHA LA ASUBUHI JULAI 18/07/2025 Tu Wachungaji Wasaidizi

  Tu Wachungaji Wasaidizi Julai 18 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.” — Mathayo 7:15 Kadiri unavyomtazama Yesu na upendo Wake usio na kifani kwa juujuu, ndivyo unavyoshindwa kubadilishwa ili kufanana Naye. Utajiona bora machoni pako mwenyewe, na hivyo kuwa na kujiamini na kuridhika na jinsi ulivyo. Ufahamu sahihi wa Yesu, kumtazama daima kama Mwanzilishi na Mkamilishaji wa imani yetu, hutupatia mtazamo wa kweli wa tabia ya Mkristo kiasi kwamba huwezi kushindwa kufanya makadirio sahihi ya maisha na tabia yako tofauti na zile za Mfano wetu mkuu. Kukamilishwa kwa ajili ya kazi yako ni shughuli ya maisha ya kila siku — kazi ngumu, mapambano ya karibu na mazoea ya kibinadamu, mielekeo ya kurithi. Inahitaji juhudi ya mara kwa mara, ya dhati na ya uangalifu ili kuitazama na kuidhibiti nafsi, kumweka Yesu kuwa mashuhuri na ubinafsi kutoonekana. Ni muhimu kuchunguza eneo dhaifu katika tabia yako, ku...

KESHA LA ASUBUHI JULAI 17/07/2025 Furaha Mwenye Dhambi Mmoja Anapotubu

  Furaha Mwenye Dhambi Mmoja Anapotubu Julai 17 “N awaambia, hivi hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.” — Luka 15:7 Yesu, Mwana wa Aliye Juu Zaidi, anashindana na nguvu za Shetani, ambaye anaweka kila mbinu iwezekanayo ili kuzuia kazi ya Mungu. Kitu cha thamani ambacho nguvu za nuru na za giza zinashindania ni nafsi ya mwanadamu. Mchungaji Mwema anatafuta kondoo Wake, na anastahimili kujikana nafsi, taabu na ufukara. Wachungaji wanajua kitu fulani kuhusu pambano hilo kali, lakini wanajua kidogo sana ukilinganisha na yale ambayo Mchungaji wa kondoo anayavumilia. Anawatafuta waliopotea kwa huruma, huzuni na kung’ang’ana. Hatimaye, Mchungaji anapompata kondoo Wake aliyepotea, anamkumbatia mikononi Mwake kwa furaha, na kumchukua mabegani Mwake ili kumrejesha zizini. Ndipo vinubi vya mbinguni vinaguswa, na wimbo wa shangwe unaimbwa juu ya fidia iliyotolewa kwa kondo...

KESHA LA ASUBUHI JULAI 16/017/2025

  Kondoo wa Kweli Wanamsikia Mchungaji wa Kweli                                         Julai 16 "Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. " — Yohana 10:16 Kweli unapaswa kuwasilishwa kwa hekima, upole na wema wa Mungu. Unapaswa kutoka kwenye moyo ambao umelainishwa na kufanywa kuwa mwenye huruma... Hebu maneno yetu yawe ya upole tunapotafuta kuongoa roho. Mungu atakuwa hekima kwake yeye atafutaye hekima kutoka kwenye chanzo cha mbinguni. Tunapaswa kutafuta fursa kila upande, tukikesha na kuomba, na kuwa tayari wakati wote ili kutoa sababu ya tumaini lililo ndani yetu, kwa upole na kicho. Tusije tukaivutia isivyofaa nafsi moja ambayo Yesu alifia; tunapaswa kudumisha mioyo yetu katika uadilifu kwa Mungu, ili fursa inapojitokeza, tupate maneno sahihi ya kusema kw...

KESHA LA ASUBUHI 15/07/2025 Kumpata Kondoo Aliyepotea

 KESHA LA ASUBUHI JULAI 15- 2025 Kumpata Kondoo Aliyepotea " Naye akimwona, amini nawaambia, humfurahia huyo zaidi kuliko wale tisini na tisa wasiopotea." — Mathayo 18:13 Yesu angependa kuhimiza thamani ya nafsi ya mwanadamu juu ya mioyo na akili za wanafunzi Wake. Anadai ushirikiano kwa shauku ya wafuasi Wake katika kuwaokoa wenye dhambi waliopotea. Kuna kondoo mmoja alipotea, idadi ndogo sana katika hesabu; na bado Yesu anamwakilisha mchungaji kuwa aachaye wale tisini na tisa, na kwenda milimani kutafuta yule mmoja aliyepotea. Sasa ni kwa nini basi wana na binti za Mungu wamebweteka, hawajali roho ambazo zinapotea karibu yao? Ni kwa nini washiriki wa kanisa wako tayari sana kuacha mzigo wote kuwa juu ya mabega ya mchungaji? Ni kosa kubwa jinsi gani, ikiwa kila raia wa neema anapaswa kuwa na sehemu ya kufanya katika kuokoa wale waliopotea. Yesu amempatia kila mtu kazi yake, na juhudi binafsi lazima ziwekwe ili kuokoa wanaopotea. Mtendakazi lazima awe na maombi mengi y...

Hatari Ya Wengi Wetu Leo Kupuuzia Sauti Ya Mungu Inayozungumza Nai Kila Uchao

Sehemu ya Kwanza   Mungu Anazungumza Kupitia Neno Lake 📖  “ Yeye anayenikataa Mimi, asiyeyakubali maneno Yangu, anaye wa kumhukumu—Neno lile nililosema ndilo litamhukumu siku ya mwisho.” .”  — Yohana 12:48 🔹 Neno la Mungu — Sauti halisi ya MUNGU Inayozungumza Yesu mwenyewe anatoa angalizo la hukumu kwa wale watakaomkataa yeye, na mhukumu aneyetajwaa hapa ni neno. kwa nini neno ndilo lihukumulo? tunaporejea (Yohana 1:1-4, 14)  Kama Neno la Mungu (Logos): Yesu ndiye ufunuo wa asili wa Mungu kwa wanadamu — si tu msemaji wa Mungu, bali Neno lenyewe . Kwa Kigiriki, "Logos" lina maana ya hekima, mantiki, na ufunuo. kama yesu ni neno pale tunapolipuuzia neno la Mungu ni dhahiri kuwa tunampuuzia Yesu mwenyewe. na somo hili litajenga msingi wa kulitambua na kuliheshimu na kufanya neno la Mungu liwe sehemu katika maisha yetu yenye tija kwa ajili ya kutuandaa na umilele.  Kila siku sauti ya aliyeumba mbingu na nchi (Mungu mwenyewe) Inazungumza. Sauti yake haitoki kwa ...

_KESHA LA ASUBUHI *JUMATATU, JULAI 14 2025*

KONDOO WALIOPOTEA NI MZIGO WA PEKEE  *Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone*?  _Luka 15:4_ ▶️ *Ni kazi muhimu sana kushughulika na akili za wanadamu. Mwanadamu ni mali ya Mungu, na malaika wanaangalia kwa shauku kubwa ili kuona namna ambavyo mwanadamu atashughulika na wanadamu wenzake.* ▶️ Viumbe wa mbinguni wanapoona wale ambao wanadai kuwa wana na binti za Mungu wakifanya jitihada kama za Kristo ili kusaidia wakosaji, wakiwaonesha roho ya upole na huruma waliotubu na walioanguka, malaika wanawakaribia, na kuwakumbusha maneno yale ambayo yatatuliza na kuinua nafsi. Malaika watakatifu wanatufuatilia kila mmoja wetu. Hatupaswi kuwadharau watu wa Mungu walio wadogo zaidi, tusitafute heshima kwa yeyote kwa ajili yetu. Malaika ni roho zihudumuzo zilizotumwa kuwahudumia wale ambao watakuwa warithi wa wokovu. Je! tutapata fadhila ya kushirikiana na wenye hekima wa mbinguni? Je!...

KESHA LA ASUBUHI JULAI 13 2025 "Yesu Alikuja Kumtafuta Kondoo Aliyepotea"

Yesu Alikuja Kumtafuta Kondoo Aliyepotea "Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu." — Luka 5:32 Yesu alipokuwa duniani alikamilisha kazi aliyokuja kuifanya—kazi ambayo ilimfanya aache kiti cha enzi cha Mungu mbinguni kwa ajili ya jamii ya wanadamu. Alitenda kazi yake ili kupitia utendaji Wake, wanadamu wainuliwe kufikia kiwango cha thamani ya kiadili mbele za Mungu. Kwa kuchukua asili ya mwanadamu, alikusudia kuiadilisha familia ya wanadamu, akiwasogeza kuwa washirika wa asili ya Mungu. Utume Wake wote ulikuwa kwa niaba ya ulimwengu uliokuwa umeasi—kutafuta kondoo aliyepotea na kumrejesha kwa Mungu. 🕊️ Sadaka ya Kiungu kwa Ulimwengu Uliopotea Bwana alituona katika hali ya kusikitisha, na akamtuma Mjumbe pekee—Yesu Kristo—ambaye angeweza kubeba hazina kuu ya msamaha na neema. Yesu, Mwana wa pekee wa Mungu, ndiye Mjumbe mwakilishi aliyewekwa wakfu kufanya kazi ambayo hata malaika wa mbinguni wasingeweza kuikamilisha. Alikuwa pekee anayeaminika kufan...